Rais
mstaafu wa awamu ya nne Mhe Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ametunukiwa
Shahada ya heshima ya udaktari wa falsafa ya mahusiano ya kimataifa jana
Jijini Dar es Salaam katika mahafaliya 30 ya Chuo Kikuu Huria Tanzania.
Mhe.
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amesema amefarijika sana kutunukiwa Shahada
hiyo ya heshima itolewayo na Chuo kikuu Huria Tanzania kwa watu ambao
wametoa mchango katika maendeleo katika jamii kupitia nafasi zao
kiutendaji.
“Naipokea
heshima hii toka Chuo Kikuu Huria Tanzania kwa moyo mmoja kwani wameona
mchango ambao nimeutoa nilipokuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kwa Awamu ya Nne hivyo basi nitaendeleza mahusiano na
ushirikiano kimataifa”.Alisema Mhe. Dkt Kikwete.
Mbali
na Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kuna baadhi ya maraisi na wakuu mbalimbali
duniani waliwahi kupata Shahada za heshima toka Chuo Kikuu Huria
Tanzania ambao ni Rais wa Awamu ya Kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere, Rais wa Awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi, Rais
wa Awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa, Rais wa zamani wa Afrika ya
Kusini Hayati Nelson Mandela na Dkt Koichiro Mastuura Mkurugenz iwa
UNESCO.
Chuo
kikuu Huria cha Tanzania kimetoa jumla ya wahitimu 69 wawili Shahada
maalum na 67 ni Shahada, Stahahada na Astashahada, ambapo Shahada ya
uzamivu ni wahitimu watatu, Shahada ya uzamili ni wahitimu 20, Shahada
wahitimu 22,Stashahada wahitimu 15 na Astashahada wahitimu 6.
Tangu
kuanzishwa kwa Chuo Kikuu Huria Tanzania mwaka 1992 jumla ya wahitimu
25,908 wametunukiwa Shahada mbalimbali na haya ni mahafali ya 30 tangu
chuo kuanzishwa
Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania Dkt Asha Rose
Migiro akimpongeza Rais mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe Dkt Jakaya Mrisho Kikwete baada
ya kumtunuku Shahada ya heshima ya udaktari
wa falsafa ya mahusiano ya kimataifa katika maafali ya 30 ya Chuo kikuu Huria Tanzania
yaliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam.
Rais mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe Dkt Jakaya Mrisho
Kikwete akiongea na wanataaluma na wageni katika maafali ya 30 ya Chuo kikuu Huria Tanzania
yaliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania Dkt Asha Rose
Migiro akifungua rasmi mahafali ya 30 ya Chuo Kikuu Huria Tanzania
yaliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam
Credit;Mpekuzi blog
0 comments:
Post a Comment