Mshukiwa wa ugaidi
ambaye amekuwa akitafutwa na polisi nchini Kenya kwa kushukiwa kuhusika
kwenye shambulizi lililoendeshwa katika chuo kikuu cha Garisa mwezi
Aprili mwaka 2015, ameuawa kwa kupigwa risasi na kikosi cha polisi cha
kupambana na ugaidi nchini Kenya.
Kulingana na Gazeti la Daily
Nation nchini Kenya ni kuwa, Suleiman Mohammed Awadh, aliuawa pamoja na
washukiwa wengine watatu wa ugaidi wakati polisi walifanya uvamizi
mapema leo asubuhi kwenye nyumba moja ya mji wa Malindi ulio pwani ya
Kenya.Gazeti hilo linasema kuwa polisi waligundua silaha, ramani ya malindi inayoonyesha maeneo ambayo walilenga kushambulia na barua iliyokuwa imeandikiwa wafadhili wa Al Shabab wakiomba pesa, nguo na chakula.
Chanzo BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment