Wednesday, 20 January 2016

Tagged Under:

Islamic State wathibitisha Jihadi John aliuawa

By: Unknown On: 04:08
  • Share The Gag
  • Jihadi John alitumiwa sana katika video za propaganda za IS
    Kundi la Islamic State limethibitisha kwamba mwanamgambo aliyetafutwa sana na mataifa ya Magharibi, aliyejulikana kama Jihadi John, alifariki.
    Kundi hilo limetangaza kifo chake kwenye jarida lake la mtandaoni kwa jina Dabiq.
    Mwanamgambo huyo aliuawa kwenye shambulio lililotekelezwa kwa kutumia ndege isiyokuwa na rubani Novemba mwaka jana.
    Marekani, baada ya kutekeleza shambulio hilo katika ngome ya IS mjini Raqqa, ilisema ilikuwa na  kwamba alikuwa ameuawa.
    Mwingereza huyo, ambaye jina lake la kuzaliwa ni Mohammed Emwazi, alionekana kwenye video nyingi za IS akiwakata shingo mateka kutoka mataifa ya Magharibi wakiwemo Waingereza David Haines, aliyekuwa mfanyakazi wa shirika la kutoa misaada, na dereva wa teksi Alan Henning.
    Kwenye tangazo la tanzia kwenye jarida hilo, Emwazi anaitwa Abu Muharib al-Muhajir, jina alilojulikana nalo katika kundi hilo.
    Maelezo ya kifo chake yanathibitisha taarifa kutoka kwa Marekani kuhusu yaliyotokea siku hiyo.
    Kundi hilo limesema Emwazi aliuawa tarehe 12 Novemba “gari alimokuwa akisafiria liliposhambuliwa na ndege isiyo na rubani katika mji wa Raqqa, ambapo gari lake liliharibiwa na akafariki papo hapo.”
    Picha ya mwanamgambo huyo akiwa ametabasamu, na ambaye anaonekana akiwa hajajifunika uso huku akiwa ameangalia chini, imechapishwa kwenye jarida hilo.
    Emwazi alizaliwa nchini Kuwait mwaka 1988 lakini akahamia Uingereza mwaka 1994 akiwa na umri wa miaka sita.

    Chanzo BBC Swahili.

    0 comments:

    Post a Comment