Msanii mkongwe wa muziki, Stara Thomas amedai kusikitishwa na kitendo
alichofanyiwa na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi aka Sugu cha
kumpita bila kumsalimia alivyokutana naye bungeni Dodoma.
Akizungumza katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio
Ijumaa hii, Stara alisema hakutegemea kutokea kwa hali hiyo kwani yeye
aliwahi kumsaidia Sugu katika kipindi cha nyuma wakati akiandaa wimbo
wake Mr II.
“Sugu anakuja nyumbani mimi nanyonyesha, ‘dada dada mimi siwezi
kufanya kazi peke yangu’” alisema. “Halafu nimekutana naye Dodoma
ananipita kama hanijui. Kitu ambacho nakumbuka Sugu na mimi tulikuwa
tunawasiliana kwenye simu akasema ‘Stara mimi nakuja na nyimbo yangu
mpya.’ Lakini alikuja kipindi ambacho mimi najifungua mtoto wangu wa
pili, nilikuwa na kama miezi miwili. Kwahiyo aliniomba ilikuwa ni ngumu
kwa sababu nilikuwa nanyonyesha, nikasema ‘any way wewe ni wangu
nikaongozana naye mpaka studio na nilikuwa narekodi huku tukipokezana
mtoto,” aliongeza Stara.
Aliongeza, “Lakini kilichoniumiza kuna wakati nilikutana naye bungeni
kiukweli hiki naomba nikiseme. Adabu aliyonionyesha Sugu ilikuwa sio.
Kwa sababu Sugu sio wa kunipita mimi bila kunisalimia, sisemi kwa ubaya
lakini kwa mtu ambaye mimi nilimpokea nikiwa na mtoto mchanga, nikaenda
naye studio na mtoto mchanga kwa mapenzi yote haijalishi hata kama kuna
mapungufu hata mpo katika vyama tofauti. Najua yule yupo kwenye chama
kingine na mimi nipo CCM, kwahiyo alionyesha zile chuki za kisiasa.”
Chanzo Bongo5
Saturday, 16 January 2016
Tagged Under:
Stara Thomas: Sikuamiani Jinsi Sugu Alivyojifanya Hanijui Bungeni
By:
Unknown
On: 22:38
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment