Tuesday, 26 January 2016

Tagged Under:

Netanyahu amshutumu Ban Ki-Moon

By: Unknown On: 23:25
  • Share The Gag
  • Benjamin Netanyahu
    Waziri mkuu wa Israel,Benjamin Netanyau amemshutumu katibu mkuu wa umoja wa mataifa,Ban Ki-Moon kwa "kuunga mkono ugaidi", baada ya kusema kuwa ni jambo la kawaida kwa watu wanaotawaliwa au kukandamizwa, kukabiliana na walowezi.
    Bw Ban alikuwa akizungumzia mzozo wa Wapalestina.
    Zaidi ya Wapalestina 155, Waisraeli 28, Mmarekani na Raia wa Eritrea wameuawa kwa kushambuliwa kwa risasi au kudungwa visu tangu Oktoba.
    "Matamshi ya katibu mkuu wa UN yanaunga mkono ugaidi," alisema Bw Netanyahu kupitia taarifa.
    "Hakuna haki kamwe kutetea ugaidi."
    Akihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Bw Ban alikuwa amesema visa hivyo vimeongezeka kutokana na kutamauka miongoni mwa Wapalestina, na hasa vijana.
    "Palestinian frustration is growing under the weight of a half century of occupation and the paralysis of the peace process," he said.
    "Kama watu wanaokandamizwa walivyoonyesha katika historia, ni kawaida kwa binadamu kukabiliana na walowezi, jambo ambalo huchochea chuki na misimamo mikali," alisema Bw Ban.
    Alieleza kuwa hatua za usalama pekee haziwezi kusitisha migogoro inayotishia amani.
    Lakini kwa mujibu wa Bw Netanyahu, Wapalestina wenyewe ndio wanaohujumu juhudi za kuundwa kwa taifa lao.
    Aidha, amesema Umoja wa Mataifa ulipoteza mwelekeo wake siku nyingi zilizopita.

    Chanzo BBC Swahili.

    0 comments:

    Post a Comment