Saturday, 16 January 2016

Tagged Under:

Tanesco yabaini wizi mkubwa migodini

By: Unknown On: 22:14
  • Share The Gag

  • Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.

    KAMATI Maalumu ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), iliyoundwa na Wizara ya Nishati na Madini, imezikatia umeme kampuni 24 za wawekezaji katika migodi ya madini ya Tanzanite, baada ya kugundua wamechezea mita zao na kulisababishia shirika hilo hasara ya zaidi ya shilingi milioni 157.
    Akizungumza jana kwenye migodi hiyo, Mwenyekiti wa kamati hiyo, John Manyema alisema kuwa zoezi hilo wamelifanya ndani ya kipindi cha Desemba 3 hadi Januari mwaka huu.
    Alisema tayari wameshatembea katika eneo la Bagamoyo, Tanga, Dar es Salaam na Manyara na kote wamebaini udanganyifu mkubwa unaofanywa na wateja wa Tanesco.
    Manyema alisema wamebaini tatizo kubwa katika migodi hiyo ni wizi mkubwa wa umeme na kuahidi kuendelea na ukaguzi mara kwa mara. “Wahusika wote tumewapa adhabu ya kuwakatia umeme katika migodi yao na kisha tumewataka kumfuata Meneja wa Tanesco Mirerani ili warekebishiwe mita zao,”alisema na kuwaonya wananchi kutojaribu kuhujumu shirika hilo kwa namna yoyote, kwani lazima watakamatwa na watapata adhabu stahiki.

    Chanzo HabariLeo.

    0 comments:

    Post a Comment