Tuesday, 26 January 2016

Tagged Under:

Zika:Obama ataka hatua za haraka kuchukuliwa

By: Unknown On: 23:47
  • Share The Gag
  • Rais Barrack Obama
    Rais wa Marekani Barack Obama ameomba hatua za haraka katika kutoa majaribio ya chanjo na matibabu dhidi ya virusi vya Zika.
    Virusi hivyo vinaambukizwa na mbu na vinasababisha dosari za maumbile.
    Bwana Obama amepokea taarifa kuhusu mulipuko wa Zika na kuna hatari Marekani ikakumbwa na visa vya virusi hivyo katika msimu wa joto.
    Virusi vya zika Rais ametaka raia wa Marekani kupata taarifa ya jinsi ya kujikinga na maambukizi hayo.
    Jumanne ya wiki hii mkaazi wa jimbo la Virginia alipatikana na virusi hivyo baada ya kuzuru nchi inayokumbwa na mruipuko wa Zika.

    Chanzo BBC Swahili.

    0 comments:

    Post a Comment