Monday, 18 January 2016

Tagged Under:

Mama Kanumba: Lulu Umenichosha, Uniache!

By: Unknown On: 22:58
  • Share The Gag
  • LULU222
    Bifu jipya! Kwa mara nyingine, baada ya kurushiana vijembe kwa muda mrefu, mama mzazi wa aliyekuwa stadi wa sinema za Kibongo, marehemu Steven Charles Kanumba ‘The Great’, Flora Mtegoa amemuonya staa wa Bongo Muvi, Elizabeth Michael ‘Lulu’ kuwa amemchosha kwa vijembe mitandaoni hivyo anamuomba amuache.
    NI KATIKA MAHOJIANO MAALUM
    Katika mahojiano maalum na Ijumaa Wikienda, mama Kanumba alisema Januari 7, mwaka huu ilikuwa ni ‘bethidei’ yake ya kutimiza umri wa miaka 60, ikiwa ni siku moja tu kabla ya ile ya Kanumba (Januari 8) hivyo kwa umri huo hataki kuendekeza mabifu na Lulu aliyekuwa mwandani wa mwanaye kabla ya kukutwa na umauti Aprili 7, 2012.
    Mama Kanumba alifunguka kuwa anamshukuru Mungu kwa kumaliza mwaka 2015 lakini hawezi kuusahau mwaka huo kutokana na mambo aliyomfanyia Lulu ambayo hapendi kuyakumbuka.
    MAMA KANUMBA LAIVU
    “Kwa sasa nina umri wa miaka 60, ni mara tatu ya umri wa Lulu. Sitaki tena malumbano na Lulu kwani amenichosha na ninachowaombeni mwaambieni aniache.
    KISA VIJEMBE MTANDAONI
    “Lulu ni mtoto mdogo sana kwangu, mara kwa mara huwa anaposti (kutumbukiza) vijembe mtandaoni akinikejeli kwa kuwa anajua situmii mitandao ya kijamii lakini ndugu zangu huwa wananiambia kunionesha kila kitu.
    “Ninachomuomba akome hiyo tabia ya kunisakama mitandaoni, kama ameamua kuvunja ukaribu na mimi aache kunidharua japokuwa mimi nilimsamehe kwa moyo mmoja lakini hajathamini hilo.
    “Lakini yote kwa yote namshukuru Mungu mwaka 2015 ulivyoisha maana ni mwaka ambao Lulu alinibadilikia na kuanza kunikosea heshima.
    MAUMIVU ZAIDI
    “Hakuna kitu kilichoniumiza kama siku aliposti mwanaume mmoja akisema kuwa huyo ndiye mtu wake wa karibu ni wazi kuwa hicho kilikuwa kijembe kwangu.
    “Pia kitendo cha kutohudhuria kumbukumbu ya kifo cha Kanumba pamoja na kwamba nilimuomba na alikubali kiliniumiza mno.
    AJUTA KUMSAMEHE
    “Niliwaza sana kuwa ni Lulu huyuhuyu aliyenifuata akanipigia magoti na kuniomba msamaha juu ya mwanangu nami nikamsamehe kwa moyo mmoja? Wakati mwingine hata najuta kumsamehe.
    “Lulu anapaswa kuangalia vitu vya kuandika mitandaoni au anyamaze kimya kwa sababu anatakiwa kujua kuwa kuna kesi ya msingi haijaisha.
    “Vizuri akakumbuka kuwa bado mimi nina maumivu na chozi la kifo cha mwanangu linanitoka hivyo asiendee kunichokonoa,” alifunga mjadala mama Kanumba.
    LULU ANASEMAJE?
    Kama ilivyo sheria ya gazeti hili kutafuta mzani wa habari, mwanahabari wetu alimtafuta Lulu kisha kumsomea tuhuma zake kutoka kwa mama Kanumba alizungumza kwa kifupi kisha akakata simu:
    “Sina cha kuzungumza kuhusu hilo kama kweli huyo mama (mama Kanumba) angekuwa na shida na mimi angenipigia mwenyewe au angeniambia nimpigie.”
    TUMEFIKAJE HAPA?
    Kanumba alifariki dunia Aprili 7, 2012 kwa kuanguka katika mazingira yaliyodaiwa kutokana na ugomvi kati yake na Lulu. Tukio hilo lilitokea nyumbani kwa Kanumba, Sinza ya Vatcan, Dar.
    Baada ya kifo hicho, Lulu alikamatwa na kuwekwa Mahabusu ya Segerea jijini Dar na baadaye kuachiwa kwa dhamana.
    Baada ya kutoka mahabusu, Lulu na mama yake, Lucresia Karugila walimfuata mama Kanumba na kuomba msamaha ambapo mama huyo aliupokea na kusema anamwona Lulu kama mtoto wake na yote ya nyuma yamepita.
    Kuanzia hapo, Lulu na mama Kanumba wakawa na ukaribu wa kindugu huku kila mwaka wakifanya kumbukumbu ya Kanumba pamoja kabla ya mwaka jana kutibuana na sasa hali ni tete.
    Chanzo: GPL

    0 comments:

    Post a Comment