Uchumi wa Uchina
ulikua kwa 6.9% mwaka jana, kikiwa kiwango cha chini zaidi cha ukuaji wa
uchumi nchini humo katika kipindi cha miaka 25.
Taifa hilo ndilo lenye uchumi wa pili kwa ukubwa duniani.Ukuaji ulipunguza kasi robo ya nne ya mwaka jana hadi 6.8%. Licha ya tangazo hilo, masoko ya hisa barani Asia hayajaathirika kwani tangazo hilo lilitarajiwa.
Wasiwasi kuhusu hali ya uchumi wa Uchina, pamoja na kupungua kwa mauzo nchi za nje na hata ndani ya nchi vimeathiri sana soko la kimataifa mwaka huu.
Kushuka kwa thamani ya sarafu ya yuan pia kumechangia kuathiri masoko.
Takwimu hizi zilizotangazwa kuhusu ukuaji wa uchumi Uchina zinaongeza shinikizo kwa Beijing kuchukua hatua kuimarisha uchumi wake.
Wasiwasi kuhusu ukuaji wa uchumi kumeilazimu benki kuu ya nchi hiyo kupunguza viwango vya riba mara sita tangu Novemba 2014.
Chanzo BBC Swahili.
0 comments:
Post a Comment