Mchekeshaji wa Orijino Komedi na mjasiriamali, Masanja Mkandamizaji
amesema kila anachomiliki amekinunua kwa pesa yake halali huku
akishangaa kwanini watu wameshtuka baada ya kuona anamiliki BMW yenye
plate namba ya jina lake.
Akizungumza katika kipindi cha 360 cha Clouds TV Ijumaa hii, Masanja
alisema anamiliki magari mengi huku akidai BMW X6 ameinunua kama mtu
mwingine anavyonunua baiskeli.
“Mimi nina magari mengi sana na yote nayachukulia kama chombo cha
usafiri cha kunitoa point moja kwenda nyingine,” alisema. “Sasa
nashangaa watu wanaongea sana kuhusu mimi kwani gari kitu gani! Hiyo BMW
X6 nimenunua kama watu wengine wanavyonunua baiskeli,” alijinadi.
Aliongeza, “Na hata hao TRA kama wananisikia waje hapa Clouds nimekuja nayo ipo hapo chini ili waangalie kama sijailipia.”
Masanja alisema anafanya biashara za aina mbalimbali hivyo kununua gari
la thamani siku kitu cha ajabu kwakuwa anaweza kununua kupitia biashara
yake moja tu.
Friday, 15 January 2016
Tagged Under:
Masanja: Nimenunua BMW X6 Kama Mtu Mwingine Anavyonunua Baiskeli
By:
Unknown
On: 23:54
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment