Shirika la habari la Al Jazeera
limefunga matangazo ya Televisheni nchini Marekani ikiwa ni chini ya
miaka mitatu tangu kuzindua huduma zake nchini humo.
Al Jazeera
imesema kuwa imelazimika kufunga matangazo yake kutokana na ugumu wa
mazingira ya soko la televisheni nchini humo. Shirika hilo lenye makao
makuu yake Qatar limesema kuwa badala yake linaimarisha na kupanua
huduma ya kimtandao katika maeneo ambayo yanaendesha mfumo huo kwa sasa.
Taarifa zinasema kuwa Al Jazeera imeshindwa kuwavutia watazamaji wa
kutosha nchini Marekani ili kuweza kujitengenezea faida.Chanzo BBC Swahili.
0 comments:
Post a Comment