Tazama Video hii Na Maelezo Ya Mh Mwigulu Nchemba Akitumbua Vijipu Uchungu huko TUNDURU, RUVUMA.
Mpekuzi blog
Ufuatiliaji wa Ugawaji wa pembejeo kwa wakulima,Nimefika wilaya ya Tunduru,Kata ya Nandembo na kata jirani kwaajili ya kujiridhisha na namna ugawaji wa pembejeo unavyofanyika kwa wakulima.
Nimekutana
na mchezo mchafu wa ugawaji wa pembejeo unaohusisha wakala wa pembejeo
kula njama na viongozi wa serikali wa kata na vijiji kuwasainisha
wakulima kuwa wamepokea pembejeo(Mbegu +Mbolea) ilia hali pembejeo hizo
zinaishia mifukoni mwa wakala.
Baadhi
ya wakulima ambao sio waaminifu wanadiriki kupokea fedha kidogo
iliwamuachie wakala zile pembejo akauze sehemu nyingine kwa bei ya juu
ili hali ni ruzuku iliyotolewa na serikali kwaajili ya kuwasaidia
wakulima kuboresha kilimo chao.
Kwa
hatua za awali kwa ubadhilifu uliofanywa na Uongozi wa kata ya Nandembo
na mawakala waliopewa dhamana kusambaza pembejeo hizo wote wamekamatwa
na jumatatu kupitia Kamati ya Ulinzi ya wilaya watapandishwa kizimbani.
Lakini kuanzia sasa wakala Bw.Zuberi Namahala na Bw.Ibrahim Mohamed Ibrahim mbali ya kukamatwa na kufikishwa mahakamani,kuanzia sasa wamefutwa kwenye orodha ya mawakala wa pembejo.
Natoa
rai kwa Viongozi,Mawakala wa pembejeo na wakulima wote popote walipo
kuhakikisha lengo la serikali la kuinua sekta ya Kilimo inafanyika kwa
uaminifu na ufanisi,kwa yeyote yule anayeshiriki kuhujumu na
kujinufaisha kupitia pembejeo zinazotolewa na serikali hatakwepa mkono
wa serikali.
Imetolewa na Mwigulu L. Nchemba,
Waziri wa Kilimo,ufugaji na uvuvi.
==>Tazama video hii Waziri wa kilimo, Ufugaji na Uvuvi, Mh Mwigulu Nchemba
akitumbua vijipu uchungu huko TUNDURU, RUVUMA....
Credit; Mpekuzi blog
0 comments:
Post a Comment