Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametengua
uteuzi na kumfukuza kazi Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Bw. Faisal Issa
kutokana na utovu mkubwa wa nidhamu aliouonesha katika kikao cha kamati
ya ulinzi kilichofanyika tarehe 15 Januari, 2016 Mjini Mwanza.
Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema Rais Magufuli amechukua hatua
hiyo baada ya kupokea taarifa ya yaliyotokea katika kikao cha kamati ya
ulinzi cha Mkoa, kilichoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa
Mulongo.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
Dar es salaam
15 Januari, 2016
Credit; Mpekuzi blog
0 comments:
Post a Comment