Meneja Uhusiano wa TCRA, Innocent Mungi
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imefungia zaidi ya vituo 20
vya redio kwa muda wa miezi mitatu kutokana na sababu mbalimbali ikiwa
ni pamoja na kushindwa kulipa ada ya leseni iliyowekwa kwa mujibu wa
taratibu zilizowekwa na mamlaka hiyo .
Vile vile mamlaka hiyo imefungia televisheni sita kutokana na sababu
hizo na adhabu hiyo imeanza Januari 18, mwaka huu. Tangi Julai, mwaka
jana TCRA ilitoa barua kwa zaidi ya watoa huduma 40 ikiwakumbusha
kulipia leseni zao.
Meneja Uhusiano wa TCRA, Innocent Mungi, alisema Septemba mwaka jana
vituo hivyo vilipewa tena onyo la kutakiwa kulipa ada kabla ya Desemba
31, mwaka jana, lakini hadi Januari mwaka huu ni watoa huduma 11
miongoni mwa vituo vilivyopewa barua ndio vilikuwa vimetimiza masharti
ya kile walichotakiwa kufanya.
Meneja huyo alisema Kifungu 22 cha Sheria Mawasiliano ya Eletroniki
na Posta cha Mwaka inaipa mamlaka kusimamisha au kufuta leseni kwa mtoa
huduma iwapo ameshindwa kulipa ada kama alivyoelekezwa.
Hata hivyo alisema kama mtu yoyote ataamua kulipa ada watamfungulia
kwa sababu adhabu inaanza Jumatatu saa sita mchana. Mungi alivitaja
baadhi ya vituo vya redio vilivyofungiwa kuwa ni Kiss FM, Radio Free
Africa, Sibuka FM, Uhuru FM, Radio Five, Breeze FM, Country FM, Ebony
Fm, Generation FM, Kili Fm, Kitulo Fm, Huruma Radio, Rock FM, Standard
FM, Top Radio, Ulanga FM, Hot FM, Impact FM, Kifimbo FM na Pride FM.
Vituo vya Televisheni vilivyofungiwa ni Star TV, Sumbawanga Municipal
TV, Tanga City TV, Iringa TV, Musa Television Network na Mbeya city TV
Akifafanua zaidi alisema baada ya miezi mitatu iwapo watoa huduma hao
watashindwa kulipia leseni zao hatua kali zaidi zitachukuliwa dhidi yao.
Hata hivyo, Mungi alikataa kubainisha ni kiasi gani cha ada ya leseni
kila mdaiwa anatakiwa kulipa na kusema suala hilo liko kati ya mamlaka
na mtua huduma.
Chanzo HabariLeo.
Saturday, 16 January 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment