Mamlaka nchini Marekani zimesema zinajaribu kuwatafuta raia wa Marekani waliopotea mjini Baghdad nchini Iraq.
Watu watatu waliopotea wanahofiwa kutekwa nyara na wanamgambo, chombo cha habari cha al-Arabiya, kimenukuu vyanzo vyake.''tuna taarifa kuhusu kupotea kwa raia wa Marekani nchini Iraq''. Maafisa wameeleza.
Msemaji wa Ubalozi wa Marekani nchini Iraq Scott Bolz amesema wanashirikiana na mamlaka za Iraq kuwatafuta.
Tukio hilo limetokea baada ya muda wa wiki moja paliposhuhudiwa kuzorota kwa hali usalama mjini Baghdad.
Wanamgambo wa Islamic state walikiri kutekeleza mashambulizi kadhaa mjini Baghdad na Dyala wiki iliyopita ambapo zaidi ya watu 50 walipoteza maisha.
Chanzo BBC Swahili.
0 comments:
Post a Comment