Tuesday, 26 January 2016

Tagged Under:

Viongozi wa UKAWA Kutoa Msimamo Wao Juu ya Suala la Zanzibar

By: Unknown On: 23:40
  • Share The Gag

  • UMOJA wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) umesema utatoa msimamo juu ya hali ya siasa ya Zanzibar baada ya kikao cha kamati tendaji kuketi na kutoa msimamo. Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe alisema hayo jana katika mkutano wake na waandishi wa habari mjini Dodoma.

    Alisema walifanya mazungumzo ya mashauriano ya hali ya siasa ya Zanzibar, yaliyohudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu wa nyama vya upinzani, wakiongozwa na aliyekuwa mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF, Maalim Seif Shariff Hamad na mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowasa.

    “Januari 28 keshokutwa kutakuwa na kamati ya utendaji na kikao hicho, kitatoa msimamo wa kitu gani kifanyike kuhusiana na siasa za Zanzibar,” alisema. Pia, alisema Baraza Kuu la Chama cha Wananchi (CUF), litatoa msimamo wake kuhusu suala la Zanzibar.

    Mbunge wa Malindi kwa tiketi ya CUF, Ally Salehe alisema wanaamini Rais John Magufuli, anaweza kuingilia mgogoro wa Zanzibar na kuupatia ufumbuzi.
    Credit;Mpekuzi blog

    1 comments: