Ingawa Shilole tayari amefunika tattoo aliyochora kifuani yenye jina la ex wake Nuh, kwa kuongeza mchoro wa ua juu yake baada ya wawili hao kuachana, Nuh Mziwanda amesema yeye bado hajaamua kufuta tattoo zake.
Nuh
ambaye alichora tattoo mbili, moja ikiwa na jina la Shishi Baby na
nyingine ikiwa na sura ya Shishi amesema kuwa endapo atapata mwanamke wa
kuziba pengo la Shishi ndio atafuta tattoo hizo.
“Mimi
sijatoa hii tattoo sababu sijapata bado mwanamke ambaye anayeweza
ku-cover nafasi ya yule mwanamke, nikipata mwanamke ambaye ataweza
kucover nafasi ya yule mwanamke, akinishawishi kweli kuona anatabia
ambazo mimi nazitaka basi…” alisema Nuh kupitia Ayo Tv
Nuh aliendelea kueleza sababu za yeye kuchora tattoo za Shishi kwenye mwili wake.
“of-course
yule mwanamke mimi nilimpenda kweli na mimi ndio nilianza kuchora
tattoo kwake yeye so I was real, nilichora tattoo kwa mapenzi sikuchora
kwasababu ya. Unajua ukichora tattoo kwasababu ya inamaanisha moyoni
unakuwa unaumia unatamani ile tattoo uitoe ndio maana hata yeye (Shishi)
aliweza kuibadilisha ikawa ua. “.
Chanzo
cha ugomvi kati ya Shilole na Nuh Mziwanda kilichopelekea penzi lao
kuvunjika kimeendelea kubaki kuwa siri yao, kutokana na wote kutotaka
kukisema licha ya Shishi kuweka wazi kuwa Nuh ndiye mkosaji.
“Sipaswi
kusema kitu gani kimetokea au kipi ambacho kimefanya mimi na bibie
tuweze kutengana kwasababu ni maisha. Katika maisha kuna kupata na
kukosa kwahiyo unaweza ukampata mtu na ukamkosa mtu, so kuachana ni
kitendo cha kawaida tu ambacho kipo katika maisha yetu ya kila siku.” Alieleza Nuh.
“Kama
yeye anasema mimi ndio nimemkosea its okay all in all najua Mungu yupo
na anatuangalia sisi binadamu tunafanya nini, mimi mama yangu
kanifundisha kaniambia mtoto wa kiume hutakiwi kuongea, mtoto wa kiume
unasifiwa kazi, kwahiyo kama yeye anasema mimi ndo nimemkosea its okay
ila moyo wake unajua kitu gani kinaendelea.” Alisema Nuh Mziwanda ambaye amekuwa kwenye uhusiano na Shishi kwa miaka mitatu.
Credit; Mpekuzi blog
0 comments:
Post a Comment