NA TUNU NASORO
UMAHIRI ulioonyeshwa na wasanii waliotumbuiza katika Tamasha jipya
la KiliFest lililofanyika kwa mara ya kwanza katika viwanja vya Leaders
jijini Dar es Salaam umeonyesha dira na mwelekeo wa tamasha kubwa zaidi
kwa
mwakani.
Tamasha hilo lililodumu takribani saa 18 baada ya kuanza saa nne
asubuhi na kumalizika saa tisa na nusu alfajiri lilipokelewa kwa shahuku
kubwa na Watanzania wapenda burudani ambao wengi wao walipongeza nia ya
tamasha
hilo, ikiwemo kulipeleka mikoa mingi zaidi kwa mwaka ujao.
Majira ya saa 11 jioni tamasha lilianza ambapo burudani kali kutoka
kwambwembwe nyingi jukwaani, Isha Mashauzi, zilianza huku shamra shamra
za mashabiki zikirindima kwa shangwe.
Baada ya Isha Mashauzi, wasanii wengine walioacha gumzo
katika tamasha hilo kwa kufanya shoo ya nzuri ni bendi ya Mapacha
Watatu, Maua, Ruby, Damian Soul, Navy Kenzo, Fid Q, Ben Paul,
Vanessa Mdee, Shettah na kundi la Weusi lililoshangiliwa kila
lilipotamka neno lililopo katika wimbo wao.
Mashabiki walionyesha kufuatilia kila kilichoimbwa kwa kufuatia
kila neno la lililoimbwa katika nyimbo za wasanii hao, huku wakiongeza
vionjo kwa kucheza kwa ustadi wa hali ya juu pamoja na wasanii wa kundi
hilo kiasi kwamba kila aliyefika katika tamasha hilo alinogewa.
“Tulidhamiria kufanya kitu kizuri na kimefanyika hivyo wapenzi
wa burudani wamelipokea na wametupa mwanga wa kuwaandalia vitu
vizuri zaidi kwa tamasha lijalo la mwakani,’’ Meneja wa Bia ya
Kilimanjaro Premium Lager, Pamela Kikuli anasema.
Kikuli anaongeza kwamba maandalizi ya tamasha hilo waliyafanya kwa muda mrefu kiasi kwamba walihakikisha kila
anayeshiriki anapata anachotarajia katika tamasha hilo
lililokuwa likishereheshwa ikwa vionjo kutoka kwa MaDJ, DJ Summer, DJ
Zero na DJ Mafuvu.
Katika kujali zaidi mashabiki wake waandaaji wa tamasha
hilo walijipanga katika mazingira yote kwa kuweka runinga
kubwa zilizowawezesha waliohudhuria kushuhudia mechi ya watani wa jadi,
Simba na Yanga, ambapo
matokeo yalikuwa Yanga 2 Simba 0.
Michezo mingine iliyokuwa ikivutia wengi ni kuimba kwa kutumia kifaa
maalumu (kilioke), mpira wa mezani (fuse ball) ambapo wengi walishinda
na wakapatiwa zawadi mbalimbali zilizoongeza chachu ya kunogesha tamasha
hilo
ambalo pia lilikuwa na viburudisho mbalimbali, ikiwemo vyakula vya kila aina na muziki na vinywaji
mbalimbali, ikiwemo bia za Kilimanjaro.
Kutimiza ahadi yao waandaaji walifanya kila lililowezekana kwa washindi waliopatikana katika michezo mbalimbali
wakajumuishwa katika mazungumzo na mastaa waliokuwepo katika tamasha hilo.
Chanzo Mtanzania
Tuesday, 6 October 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment