MGOMBEA ubunge wa Segerea, Dar es Salaam kwa tiketi ya Chama cha
Wananchi (CUF), Julius Mtatiro amesema atahakikisha wanavunja makufuli
yote.
“ Naombeni wananchi tuseme Magufuli…no, in one…kwa miaka yote katika
jimbo hili hakuna huduma muhimu ya maji, miundombinu..iwe jua au mvua
barabara hazipitiki bado CCM wanataka tuwapeleke Ikulu
haiwezekani,”alisema Mtatiro.
Alisema mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli alikuwa wizara
inayoshughulika na ujenzi lakini matokeo yake ameshindwa kutengeneza
barabara za Segerea sasa anaomba aende Ikulu akafanye nini, apumzike tu!
“Ndugu zangu ilani ya UKAWA ndiyo suluhisho la kero zetu ifikapo
Oktoba 25, mwaka huu kura zote wapeni wagombea wa UKAWA,”alisema
Mtatiro.
Mtatiro alisema kuna mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM,
Bonna Kalua, amekuwa akipita na mikoba kugawa fedha kwa wananchi.
Alisema watakachokifanya sasa ni kumvizia na kumpora mkoba huo kisha
fedha hizo kugawa kwa vijana na wanawake wanaoteseka kila kukicha.
“Sisi hatuna mashindano ya urembo… tena mwambieni tukiunasa mkoba
wake kwa sasa kazi anayo… fedha zote tutagawa kwa wenye shida,”alisema
Mtatiro.
TAMBWE HIZA
Naye aliyekuwa Ofisa katika Kitengo cha Propaganda cha CCM, Tambwe
Hiza akiwa katika mkutano uliofanyika kwenye uwanja wa TP Uzuri,
alieleza kushangazwa kwa kitendo cha Didas Masaburi (aliyekuwa meya wa
Dar es Salaam) kugombea ubunge.
“Jambo baya mnalofanyiwa wananchi wa Sinza, Ubungo… yaani wale ambao wamewafanyia mabaya ndiyo wamewaleta kuwa wagombea wenu.
“Eti Masaburi anagombeaubunge muone jinsi watu hawa walivyo na dharau, ”alisema.
Tundu Lissu
Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu, amemtaka Rais Jakaya
Kikwete kutoa msimamo wake kuhusu kauli iliyotolewa na Mwenyekiti wa
Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Bulembo kuwa
chama hicho hakiko tayari kukabidhi Ikulu kwa upinzani.
Alisema ikiwa Rais Kikwete atakuwa upande wa kiongozi wake, wanachama
wa Ukawa kama watakuwa wameshinda Oktoba 25 mwaka huu, watakwenda moja
kwa moja Ikulu kwa nguvu ya umma kudai ushindi wao.
“Katika nchi yetu sheria zetu hazina utaratibu hivyo tunamtaka Jakaya
(Rais Kikwete) atwambie ni utaratibu upi atatumia kutukabidhi serikali
pamoja na ratiba nzima ya kufanya hivyo.
“Endapo tutashinda halafu wakashindwa kuondoka tutakwenda hadi Ikulu kudai ushindi,” alisema.
Created by Gazeti Mtanzania.
Saturday, 3 October 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment