Saturday, 3 October 2015

Tagged Under:

Wanajeshi 7 wafa kwa ajali

By: Unknown On: 00:10
  • Share The Gag
  • Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na wapiganaji wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Bulombora wakitoa heshima wakati wa kuaga miili ya vijana wa JKT waliokufa kwa ajali ya gari mjini Kigoma juzi.

    VIJANA Saba wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), kikosi cha 821 Bulombora wilayani Uvinza mkoani Kigoma, wamefariki dunia na wengine 22 wamejeruhiwa wengi wao vibaya baada ya gari walilokuwa wakiafiria kupinduka.
    Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Mkoa Kigoma, Kanali Mamdadi Kisui amesema wapiganaji hao walikutwa na mauti juzi saa 10 jioni katika eneo la Mlima Pasua nje kidogo ya Manispaa ya Kigoma Ujiji.
    Kanali Kisui alisema wapiganaji hao walikuwa wakisafiri na gari la Jeshi aina ya Iveco lenye namba za usajili 5717 JW 09 lililokuwa likitokea Kambi ya Burombola, kwenda mjini Kigoma likiwa na vijana 30 wa JKT.
    Akijibu maswali ya waandishi, Kanali Kisui alisema vijana hao ni sehemu ya vijana waliojiunga na JKT baada ya kuhitimu elimu ya kidato cha sita, lakini baada ya kumaliza mafunzo ya Jeshi, wakaomba kubakia kambini wakisubiri taratibu za kujiunga na elimu ya juu.
    Naye mganga mfawidhi wa hospitali ya Mkoa Kigoma Maweni, Dk Fadhili Kibaya alitaja askali waliofariki katika ajali hiyo kuwa Ally Kambagwa, Mkazi wa Mtwara, Abeli Maisha mkazi wa Morogoro na Eugini Bitati, mkazi wa Kibondo Mkoani Kigoma.
    Wengine ni pamoja na Saidi Sadara, mkazi wa Kahama mkoani Shinyanga, Bakari Kibaya mkazi wa Tanga na Fredric Kaemela mkazi wa Njiro mkoani Arusha. Mganga huyo mfawidhi alitaja majeruhi wa ajali hiyo kuwa ni Benedict Ndokeye, Raphaeli Johanna, Athanasi Emanuel, Abui Nzoge, Abubakari Peter, Abubakari Msubi, Deusi Manyanya, Edward Nyanda na Eliasi Magesa.
    Wengine ni pamoja na Geofly Maliki, King Kasefu, Kamiliusi Agida, Lameck John, Martini Kupatu, Stevin Denis, Saidi Omary, Saidi Zuberi, Shabani Zakaria, Victor Saverxy, Jackson Nyarubu na Muhamed Nyimbo.
    Vijana hao wa JKT waliagwa jana jioni katika Hospitali ya Mkoa Kigoma na baadaye walisafirishwa kwenda katika mikoa yao kwa maziko ambapo Katibu Tawala wa Mkoa Kigoma, John Ngunguru aliongoza viongozi wa Serikali na Kamati ya Ulinzi ya Usalama kuaga na kuwasindikiza akimwakilisha Mkuu wa Mkoa Kigoma, Issa Machibya ambaye yuko nje ya mkoa kikazi.
    Katika salamu zake kwa niaba ya Serikali, Ndunguru alisema Serikali imesikitishwa na ajali hiyo na ni pigo kubwa kwao kwani vijana hao walikuwa nguvu kazi na viongozi wa Taifa katika siku chache zijazo na wamekutwa na mauti akiwa chuoni wakipikwa kwa ajili ya kulitumikia Taifa.
    Akitoa salamu kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali David Mwamunyange, Mkuu wa Jeshi Mkoa Kigoma, Kanali Mamdad Kisui alisema mkuu wa majeshi amepokea kwa masikitiko makubwa msiba huo ameungana na ndugu na jamaa katika kuombeleza msiba huo.

    Created by Gazeti la HabariLeo.


    0 comments:

    Post a Comment