MKURUGENZI wa Jerusalem Film Company, Jacob Stephen ‘JB’ ameweka wazi
kuwa kamwe hafikirii kuwa mwanasiasa kwani sanaa inamlipa zaidi.
Akizungumza na mwanahabari wetu katika mahojiano mafupi, JB alisema
kipindi cha nyuma ziliibuka tetesi kuwa huenda anaweza kuwa mwanasiasa
lakini ukweli kutoka moyoni, sanaa inamlipa.
“Sanaa inanilipa, sifikirii kama ubunge au siasa kwa ujumla inaweza
kunilipa kama sanaa ambayo naipenda kutoka moyoni. Labda nikupe mfano,
kupitia kampuni yangu, nikizalisha filamu moja inatoa ajira kwa
wafanyakazi wasiopungua 30, itatoa ajira katika maduka, machinga na
sehemu mbalimbali zinazouzwa filamu.
“Sanaa imetoa ajira kwa wasanii Mil 10. Unafikiri hao watu wangefanya nini kama si sanaa?,” alisema JB.
JB aliongeza kuwa, kwa sasa anamuunga mkono mgombea urais wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM), John Magufuli kwani mwenyekiti wa chama hicho,
Jakaya Kikwete ameweka misingi mizuri katika sanaa.
“Kikwete ametusaidia kwa kiasi kikubwa kuitangaza sanaa yetu, amekuwa
akishiriki katika shughuli zetu kitu ambacho kwetu sisi kina maana
kubwa sana katika suala zima la kututangaza na ndiyo maana tunaunga
mkono CCM na ukizingatia Ilani ya CCM ya uchaguzi huu, imetugusa moja
kwa moja,” alimalizia JB.
Chanzo: GPL
Tuesday, 6 October 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment