MWONGOZAJI bora wa filamu mwenye tuzo ya ZIFF 2015, Honeymoon
Aljabri, yupo mbioni kukamilisha filamu yake ya pili ya ‘Forgotten Hero’
mwishoni mwa mwaka huu.
Mwongozaji huyo Mtanzania anayeishi Houston, Marekani, aliliambia
MTANZANIA kwamba ameandika na kuiongoza filamu yake hiyo nchini
Marekani, huku akidai kwamba ujumbe katika filamu hiyo unaonyesha
uhusiano wa wapendanao ambao mmoja wao aliwahi kushiriki vita.
“Nimeiandika na kuiongoza filamu hii kupitia kampuni yangu ya Motion
Art Production na sasa nimeshanza kuisambaza matangazo yake, natumaini
itafanya vizuri na kuwa mwongozo bora tena na wa kuigwa na waongozaji
wengine wenye hofu ya kuwaongoza wasanii maarufu, wakiwemo kutoka
Marekani kama nilivyofanya katika filamu hii,’’ alieleza Honeymoon.
Honeymoon alishikilia tuzo ya muongozaji bora wa filamu na filamu
yake ya ‘Daddy’s Wedding’ ikatunukiwa tuzo ya filamu yenye picha bora
mwaka 2015, wakati wa tamasha la filamu za nchi za majahazi (ZIFF).
Chanzo: Mtanzania
Tuesday, 6 October 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment