LOS ANGELES, MAREKANI
ALIYEKUWA mpenzi wa zamani wa msanii wa hip hop nchini Marekani, Kanye West, Amber Rose, juzi alidondosha
chozi baada ya kukumbuka maneno ya Kanye West pindi walipokuwa wapenzi.
Februari mwaka huu Kanye West kupitia radio ya Power 105.1 kwenye
kipindi cha The Breakfast Club ya nchini Marekani, alisikika akisema
kuwa ‘Ni vigumu kuishi na mwanamke kama Amber Rose, hata
wanawake wenzake inakuwa ngumu, baada ya kuachana naye nilitumia nusu
saa kumfikiria Kim Kardashian.’
Mrembo huyo alikumbuka kauli hiyo alipokutana na wanawake mbalimbali jijini Los Angeles kwa ajili ya kujadili
maendeleo ya wanawake badala yake akajikuta akibubujikwa na machozi
“Siwezi kumsahau Kanye West kutokana na maneno yake, lakini
nimemsamehe kwa kuwa mimi nibinadamu, nilimpenda lakini
hatukudumu,” alisema Amber Rose.
Chanzo Gazeti la Mtanzania
Tuesday, 6 October 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment