Tuesday, 6 October 2015

Tagged Under:

Magufuli ammwagia sifa Dk. Willbrod Slaa

By: Unknown On: 04:19
  • Share The Gag
  • NA BAKARI KIMWANGA, HANANG’ KWAANGW’ MGOMBEA urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli amemsifu aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbrod Slaa na kusema ni kiongozi safi anayewapenda Watanzania.
    Alisema kama Dk. Slaa, angekuwa anagombea nafasi yoyote angewaambia Watanzania ni mtu safi mwenye uchungu na taifa lake.
    Dk. Magufuli, alitoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti jana katika mikutano yake ya kampeni aliyoifanya majimbo ya Hanang’, Mbulu Vijijini, Mbulu Mjini na Karatu.
    Alisema anaona fahari nchi kuwa na viongozi kama Dk. Slaa. “Mimi situkani mtu yeyote au chama chochote ila kama
    angekuwa anagombea Dk. Slaa ningewaambia mumchague kwa sababu ni kiongozi safi sana mwenye uchungu na Taifa lake.
    “Kwa kuwa hayupo, nawaaomba mkichague CCM, mnipe kura mimi Magufuli pia mnichagulie wabunge na madiwani wa CCM,” alisema Dk. Magufuli.
    Katika hatua nyingine, Dk. Magufuli alimwomba Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye ampigie kura katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25. Dk. Magufuli alitoa kauli hiyo, baada ya kutua katika Wilaya ya Hanang’ mkoani Manyara na kufanya mkutano katika Kijiji cha Endasak nyumbani kwao na Sumaye.
    Amesema pamoja na kuondoka Sumaye ndani ya CCM, bado anawajibu wa kumwomba kura yake pamoja na Watanzania wote ili wamchague.Sumaye ambaye alikuwanwaziri mkuu kwa miaka 10 katika utawala wa Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, alihama CCM na kujiunga na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) hivi karibuni.
    Dk. Magufuli aliwasili wilayani Hanang’ juzi jioni, akitokea Babati, huku akisimamishwa na wananchi wa eneo la Endasak ambao walikuwa makundi mawili ya Chadema na CCM.
    Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Katesh wilayani hapa jana, Dk. Magufuli alisema anajua
    changamoto za wilaya hiyo, licha ya baadhi ya viogozi waliokuwapo serikalini kuzikana na kusema hakuna kilichofanyika.
    Alisema suala la ujenzi wa barabara ilikuwa ni moja ya kazi aliyokuwa akiisimamia kwa kutumwa na rais na sasa anahitaji naye kuwatuma wasaidizi wake, wakiwamo mawaziri ili wamalizie viporo vilivyobaki.
    “Mimi si mnaniita tingatinga, niwezesheni kwa kunichagua niwe rais ili nitinge hadi Ikulu. Jana (juzi), jioni nilisimamishwa pale Endasak alipozaliwa mmoja wa mawaziri mkuu (Sumaye) ambaye aliondoka kwenda Ukawa nikaomba kura yake,” alisema Dk. Magufuli.

    Chanzo Gazeti la Mtanzania

    0 comments:

    Post a Comment