Tuesday, 6 October 2015

Tagged Under:

Shilole aandaa kolabo ya hatari

By: Unknown On: 23:49
  • Share The Gag


  • MWANADADA nyota wa muziki wa mduara, Zuwena Muhamed ‘Shilole’ amesema yupo katika mpango wa kufanya muziki kwa kushirikiana na nyota wa Nigeria, Yemi Alade.
    Akizungumza Dar es Salaam jana alisema mambo yapo katika hatua nzuri na atatoa taarifa kwa wapenzi wa kazi zake kwaajili ya ujio wa kazi mpya.
    “Yemi ni msanii mkubwa sana na anavitu vingi lakini tumefikia hatua nzuri ya mazungumzo naamini ujio wa kazi yangu nitakayoshirikiana na mwanadada huyo muda mchache kuanzia sasa,” alisema.
    Shilole alisema watu wake wanaomfanyia mpango wa kufanya kazi na mwanadada huyo wanaendelea na mazungumzo na wamemwambia wapo katika hatua nzuri.
    “Nawaomba wapenzi wa kazi zangu waendelee kukaa tayari kwa ujio huo wa kimataifa na nawahakikishia siwezi kuwaangusha katika hilo kwani naamimi ndoto zangu ni kuhakikisha nafika kimataifa,” alisema.

    0 comments:

    Post a Comment