Ndege za kijeshi za Jeshi la Wananchi wa Tanzania, JWTZ.
MARUBANI wawili wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), wanahofiwa kufa
maji baada ya ndege yao ya mazoezi, kuangukia katika mwambao wa Bahari
ya Hindi eneo la Visiwa vya Mbudya, Kaskazini Mashariki mwa Jiji la Dar
es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kurugenzi ya Habari na Mahusiano ya JWTZ
Makao Makuu, ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa 3.30 asubuhi.
Ilisema mara baada ya ajali hiyo, marubani wake, Luteni Kanali Talkisiyo
Bruno Ndongoro na Kapteni Gaudence Peter Hamis walipotea.
Taarifa hiyo iliongeza kuwa, chanzo cha ajali hiyo ni hitilafu ya
injini, jambo ambalo limeelezwa marubani hao walipoligundua, walifanya
juhudi za kujiokoa kutoka katika ndege hiyo, kwa bahati mbaya
waliangukia baharini na kuzama. Kutokana na tukio hilo, JWTZ imetoa
taarifa ikisema inaendelea kuwatafuta marubani hao kwa kutumia boti za
kijeshi.
Created by Gazeti la HabariLeo.
Saturday, 3 October 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment