Saturday, 3 October 2015

Tagged Under:

Kikwete azindua usajili biashara kwa mtandao

By: Unknown On: 00:34
  • Share The Gag
  • Raisi Jakaya Kikwete akizinduamfumo wa usajil wa majina ya wafanyabiashara kwanjia ya mtandao wakati wa Kikao cha Tisa cha Baraza la Taifa la Biashara nchini (TNBC) kilichofanyika Ikulu, Dar es Salaam jana. Wengine ni Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (kushoto) na Mwenyekiti wa taasisi ya secta binafsi nchini (TPSF), Reginald Mengi.

    RAIS Jakaya Kikwete amezindua huduma ya usajili jina la biashara kwa njia ya mtandao inayotolewa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni Nchini (BRELA), ambayo imeondoa mazingira ya rushwa na kuokoa muda.
    Uzinduzi huo ulifanywa jijini Dar es Salaam jana kwenye mkutano wa tisa wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), lililokaa na kupokea taarifa za utekelezaji wa majukumu waliyokubaliana kwenye mkutano wa nane uliofanyika mapema mwezi Septemba.
    Akizungumzia huduma hiyo ya usajili jina la biashara kwa njia ya mtandao, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Brela, Frank Kanyusi alisema kuzinduliwa rasmi kwa huduma hiyo, kutaondoa mianya ya rushwa na kuokoa muda wa wafanyabiashara, ambao awali iliwalazimu kuifuata Brela.
    “Tumefanikiwa kuzindua huduma hii ya usajili kwa njia ya mtandao, ni wazi kwamba yale malalamiko ya rushwa kwa watumishi wetu yameondoka, kwa maana sasa unasajili ukiwa huko ulipo na cheti chako utaletewa ulipo,” alisema Kinyusi.
    Alisema huduma hiyo ni mafanikio kwao na faida kwa wafanyabiashara, ambao awali walilalamikia mfumo wa kusajili kampuni, ambao wakati mwingine iliwalazimu kutumia muda mrefu hadi siku kadhaa, kusajili. Kinyusi aliongeza kwamba huduma hiyo ilianza kutumika Julai mwaka huu.
    Alisema hadi sasa ni miezi mitatu na tayari wamesasajili majina ya kibiashara zaidi ya 1,000.

    Created by Gazeti la HabariLeo.

    0 comments:

    Post a Comment