Merehemu Mchungaji Christopher Mtikila |
Mwanasiasa mkongwe na Mwenyekiti wa Chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila amefariki dunia leo alfajiri kwa ajali ya gari katika Kijiji cha Msolwa, Chalinze.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Jaffar Mohamed amethibitisha na kuongeza kuwa Mtikila alikuwa akitokea Morogoro kuelekea Dar es Salaam.
Amesema chanzo cha ajali hiyo bado kinachunguzwa.
Taarifa zaidi zitakujia hivi punde.
Chanzo Gazeti la HabariLeo.
0 comments:
Post a Comment