Sunday, 4 October 2015

Tagged Under:

Matamko ya Rais yavuruga mkutano

By: Unknown On: 06:04
  • Share The Gag

  • Mkuu wa Mkoa wa Kagera, John Mongella.

    MKUTANO Mkuu wa Chama cha Wauguzi nchini (TANNA) umeahirisha ghafla kwa kile kinachoelezwa kuwa ni sababu za kiusalama kufuatia baadhi ya wajumbe wa mkutano huo kutofautiana kuhusiana na kauli iliyotolewa na Rais wa Chama hicho Paul Magesa kuwa chama hicho kinaunga mkono vuguvugu la mabadiliko kuelekea uchaguzi mkuu ujao.
    Kauli hiyo ilitolewa na Rais wa Chama cha Wauguzi nchini (TANNA) Magesa na kusababisha kikao cha Baraza Kuu la Wauguzi kinachoendelea mjini Bukoba kuzua sintofahamu kubwa miongoni mwa wajumbe wake katika siku yake ya tatu iliyokuwa na ajenda ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa chama hicho.
    Rais huyo alizua sintofahamu baada ya kutoa kauli hiyo tata alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Bukoba baada ya ufunguzi wa mkutano wao wa siku tatu ulioanza Oktoba Mosi mwaka huu na kufunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera John Mongella na baada ya ufunguzi huo Magesa aliitisha kikao kidogo mbali na mkutano na kutoa tamko hilo lililozua tafrani miongoni mwa wajumbe wenzake.
    Kaimu Muuguzi Mkuu wa Serikali Daktari Anna Kasangala akikemea kauli iliyotolewa na Rais wa chama hicho ya kudai kuunga mkono vuguvugu la mabadiliko kuelekea katika uchaguzi mkuu nchini, ni kauli binafsi na sio kauli ya chama kama ilivyokaririwa na baadhi ya vyombo vya habari hapa nchini.

    Chanzo Gazeti la HabariLeo.

    0 comments:

    Post a Comment