MKURUGENZI wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Lwakatare akihutubia mkutano wa hadhara.
MKURUGENZI wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), Wilfred Lwakatare jana alishindwa kufika katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu, kusikiliza kesi ya kujaribu kudhuru kwa sumu
inayomkabili pamoja na Ludovick Joseph.
Kesi hiyo ilitajwa jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba,
ambapo Wakili wa Serikali Lilian Itemba alidai kuwa upelelezi
haujakamilika pia Lwakatare hajafika mahakamani. Hakimu Simba alisema
amepata barua kutoka kwa mshitakiwa huyo na kuhoji kama upande wa
Jamhuri pia umeipata barua.
Wakili Itemba alidai kuwa, wamepata barua kutoka kwa Lwakatare
akiomba ruhusa, lakini hawajui kama mahakama ina taarifa na imetoa
ruhusa kwa mshitakiwa huyo.
Katika kesi hiyo, Lwakatare na Ludovick wanadaiwa kuwa Desemba 28,
2013 katika eneo la King’ongo, Wilaya ya Kinondoni, kwa pamoja walikula
njama za kujaribu kumdhuru aliyekuwa Mhariri wa Gazeti la Mwananchi
Dennis Msacky kwa njia ya sumu. Kwa sasa Msacky ni Mhariri Mtendaji wa
gazeti la Mtanzania.
Chanzo gazeti la Habari Leo.
Tuesday, 6 October 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment