Tuesday, 6 October 2015

Tagged Under:

‘Iko haja kuangalia utaratibu wa Hija’

By: Unknown On: 03:46
  • Share The Gag

  • Mufti wa Tanzania, Alhaji Abubakar Zubeir.

    WAKATI Watanzania wakiendelea kuomboleza vifo vya mahujaji wanane na wengine waliojeruhiwa huko nchini Saudia Arabia, Mufti wa Tanzania, Shehe Abubakari Zuberi ameiomba serikali kuangalia utaratibu wa kuzungumza na Saudia ili kuweka utaratibu mzuri wa ibada ya Hijja utakaosaidia kuepukana na madhara yaliyojitokeza mwaka huu kutokana na kufungwa kwa njia moja.
    Aidha, amesema amezungumza na shirikisho la Taasisi za Hijja Tanzania, kuhakikisha wanayachukua mapungufu yaliyojitokeza kwenye Hijja mwaka huu na kuyawasilisha kwenye mikutano ya Saudi Arabia ili kuhakikisha madhara kama hayo hayajitokezi tena.
    Akizungumza na jana jijini Dar es Salaam, Mufti Zuberi alisema mapungufu makubwa yaliyojitokeza katika ibada hiyo ni kufungwa kwa njia moja ya kuelekea eneo la Jamaratul Aqaba na kusababisha kutumika njia moja kwenda na kurudi.
    Alisema hali hiyo ilisababisha msongamano na watu kukanyagana na kusababisha maafa makubwa ambapo katika hali ya kujiokoa wengine walipoteza maisha, wengine ni majeruhi na wengine hawajulikani walipo hadi sasa.
    “Mwaka huu Tanzania tulipata mahujaji 3,000 ila hatuwezi kuwa na taarifa sahihi kwa kuwa wengine bado hawajarudi na kila wakala anautaratibu wake. Hijja za Tanzania hazieleweki tofauti na nchi zingine, unaweza ukakuta kesho safari mtu ndo anajitokeza leo,” alisema.
    Alisema waliofariki hadi sasa ni nane na 35 ambao hawajaonekana hawezi kuthibitisha kwa sasa kwamba wamekufa ila wanasubiri uchunguzi zaidi na taarifa itatolewa hapo baadaye kwa kuwa kuna watu pia walienda kwa njia za panya.

    Chanzo Gazeti la HabariLeo.

    0 comments:

    Post a Comment