Kocha Mkuu wa Yanga, Hans Van De Pluijm.
KOCHA Mkuu wa Yanga Hans van Pluijm ametamba kuwa haoni sababu ya
kushindwa kutetea ubingwa wake. Yanga ndio inaongoza ligi hiyo ikiwa na
pointi 15 na katikati ya wiki hii iliifunga Mtibwa Sugar mabao 2-0
kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Akizungumza na gazeti hili jana, Pluijm alisema mechi zilizokuwa
zikimuumiza kichwa ni Simba na Mtibwa na amezishinda hivyo haoni sababu
ya kutotetea ubingwa. "Simba kutokana na historia ya kukutana na Yanga
na kuifunga nilikuwa naihofia, na Mtibwa nilihofia maana uwanja wa
Jamhuri huwa mgumu kwa Yanga, sasa tumeshinda na tuna imani tutashinda
mechi zote zilizosalia," alisema kocha huyo raia wa Uholanzi.
Aidha alisema, anafahamu ugumu wa mechi zilizosalia kwani sasa kila
timu inayokutana nayo itakamia lakini anaamini atashinda. "Mikakati
yangu na timu yangu ni kushinda mechi zote katika raundi hii ya kwanza,
karibu timu zote sumbufu tumezishinda naamini huko kulikobaki
tunateremka tu," alisema.
"Lakini si kwamba nazizarau timu nyingine hapana, najua mambo
yatazidi kuwa magumu maana sasa kila timu itataka kuifunga Yanga na hapo
ndipo ugumu unapokuja, lakini nina timu nzuri, tutashinda mechi zote na
kutetea ubingwa wetu," alisema.
Chanzo Gazeti la HabariLeo.
Sunday, 4 October 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment