Wednesday, 7 October 2015
Tagged Under:
NA MWANDISHI WETU, PEMBA
MGOMBEA urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad amesema ana matumaini makubwa uchaguzi utafanyika kwa amani na utulivu licha ya kauli za baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuashiria kuvurugwa amani na umoja wa kitaifa kwa wananchi wa Zanzibar.
Maalim Seif alitoa tamko hilo alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara wa kampeni katika majimbo ya Chakechake na Wawi uliofanyika katika uwanja wa Ditia Wawi, kisiwani Pemba jana.
Alisema kauli zinazotolewa na viongozi wa CCM Zanzibar kwamba CUF kinajiandaa kufanya vurugu ifakapo Oktoba 22 hadi 24 ni vita vya kisaikolojia inayo lenga kuwatisha wananchi na hasa wapinzani ili waogope na wasijitokeze kwa wingi kwenda kupita kura siku ya uchaguzi mkuu.
Mgombea huyo alisema anashangaa kuona hadi leo viongozi hao wa CCM bado wana fikra za kizamani za kuwatisha wananchi, ikiwemo madai wanayotoa kuwa, Maalim Seif akichaguliwa kuwa Rais wa atamrejesha Sultan wa Zanzibar.
“Wananchi nakuombeni zipuuzeni kauli hizo, hivyo ni vita vya kisaikolojia nawahakikishia tutafanya uchaguzi kwa amani, kura zitahesabiwa kwa amani na mimi nitatangazwa kuwa Rais wa Zanzibar kwa amani bila vurugu”,
alitamba Maalim Seif maarufu ‘Simba wanyika’.
Maalim Seif alisema viongozi hao wa CCM wanawatia hofu bure wananchi kwa sababu chini ya Serikali atakayoiongoza itakuwa ni ya Wazanzibari wenyewe na hakutakuwa na amri kutoka sehemu yoyote.
“Wananchi wakinichagua watatukabidhi Serikali wenyewe watupe nafasi kuifanya Zanzibar Singapore ya Afrika sawa.. sawasawa”, aliuliza Maalim Seif.
Katika mkutano huo, mgombea Ubunge wa Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC) jimbo la Chonga, Hamad Khamis Hamad alikihama chama chake na kuhamia CUF.
Hamad pamoja na wanachama wengine 69 kutoka ADC na CCM walikabidhiwa kadi za CUF na Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad.
Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la CUF, Mohammed Ibrahim Sanya akizungumza katika mkutano huo wa hadhara aliwataka wananchi wa Pemba wasifanye makosa kuwachagua viongozi wa CCM kwa sababu hawana uwezo tena wa kuwaletea maendeleo, badala yake kura zao wampe mgombea huyo wa CUF ili aweze kuwatatulia kero na ugumu wa maisha.
Created by Gazeti la Mtanzania
Maalim Seif acharuka Zanzibar
By:
Unknown
On: 07:18

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment