Katika hotuba yake
iliyojaa kila aina ya hisia kali, Rais Obama amebainisha wazi mipango
yake juu ya kuweka mikakati thabiti ya udhibiti silaha za moto, akisema
kwamba Marekani haipaswi kukubali mauaji kama gharama ya uhuru.
Obama
amesema kwamba hatua madhubuti zinapaswa kuchukuliwa ambazo
zitajumuisha ufuatiliaji wa tangu awali wa upatikanaji silaha, pia
uchunguzi wa afya ya akili utazingatiwa na hii ni pamoja na kumbukumbu
za uhalifu wa mtuhumiwa zitahusishwa pia.Pamoja na machozi yaliyokuwa yanashuka njia mbili juu ya mashavu ya Rais Barack Obama, amesema suala la upatikanaji wa silaha lilikuwa limeliteka nyara bunge la Congress, lakini suala hilo halitaiteka nyara Marekani yote wakati huu ambapo uhalifu wa silaha umeua wamarekani wengi mno ukilinganisha na ajali za barabarani.
Rais Obama anatarajiwa kuweka hadharani hatua zitakazochukuliwa dhidi ya matumizi mabaya ya silaha na hasa ikizingatiwa hii ni miaka ya upinzani mkali katika serikali yake.
Lakini chama cha wauza silaha nchini Marekani kilichoundwa mnamo mwaka 1871, chenye kufuatilia matumizi salama ya silaha na usalama wa silaha nchini Marekani na pia hutetea haki ya kuwa na silaha ama kuibeba wamekosoa hotuba ya Rais na kusema kwamba mapendekezo yake hayatazuia mauaji ya halaiki kutokana na aliyoyasema katika hotuba yake.
Created by BBC Swahili.
0 comments:
Post a Comment