MAMLAKA ya Mapato (TRA) imeshakusanya Sh bilioni 11.9 kutoka kwa
wafanyabiashara waliokuwa wamekwepa kulipa kodi. Kiasi hicho ni sehemu
ya Sh bilioni 80 zinazotakiwa kukusanywa kutoka kwa wafanyabiashara hao
wanaodaiwa waliondosha kontena katika bandari za nchi kavu kinyume cha
taratibu za forodha.
Hata hivyo, kampuni 19 za wafanyabiashara hao waliopewa siku saba na
Rais John Magufuli wawe wamelipa kodi baada ya kubainika kuhusika
kukwepa kodi katika sakata la utoroshaji wa kontena 329 kutoka katika
baadhi ya bandari kavu, hawajalipa kodi hiyo wakidaiwa kugoma kulipa
adhabu.
Hayo yalielezwa jana jijini Dar es Salaam Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA,
Alphayo Kidata katika mkutano na waandishi wa habari ambako pia alisema
mamlaka imevunja rekodi ya ukusanyaji kodi baada ya kukusanya Sh
trilioni 1.4 Desemba mwaka jana kutoka Sh trilioni 1.3 za Novemba 2015.
Waliogomea adhabu “Hizi kampuni zingine 19 sio kwamba wamegoma kulipa
kodi, ila wameomba wafanye reconciliation (mlinganisho) ya miamala na
TRA kuhusu kiasi ambacho wanatakiwa kulipa. Wanachogomea kulipa ni zile
adhabu ambazo wanatakiwa kuzilipa kwa kukwepa kodi,” alisema Kidata.
Kidata alisema Sh bilioni 80 zinatakiwa kulipwa na wafanyabiashara
hao ambao waliondosha kontena katika bandari za nchi kavu bila kulipa
ushuru. Siku ya mwisho ambayo iliwekwa na Rais Magufuli ilikuwa Desemba
12.
Baada ya kubainika kuwepo kwa upotevu huo, TRA iliwaandikia hati ya
malipo inayowataka wafanyabiashara hao kulipa kodi stahiki pamoja na
adhabu. Baadhi ya wafanyabiashara wanadai kuwa walishalipa kodi hiyo
kupitia kwa mawakala ambao baadhi yao wametoroka hivyo kuwataka walipe
adhabu ni kuwaonea.
Wavuka rekodi Katika hatua nyingine, TRA imevunja rekodi ya
ukusanyaji wa kodi baada ya kukusanya Sh trilioni 1.4 Desemba mwaka jana
kutoka Sh triKidata alisema katika kipindi cha Julai hadi Desemba,
mamlaka yake imekusanya Sh trilioni 6.4 ikilinganishwa na lengo ambalo
lilikuwa ni kukusanya Sh trilioni 6.6 ambazo ni sawa na asilimia 95.5 ya
makusanyo yote.
Kidata alisema kuongezeka kwa makusanyo ya kodi katika kipindi hiki
kunatokana na mikakati madhubuti ambayo TRA imeiweka tangu Serikali ya
awamu ya tano iingie madarakani .
Pikipiki Akizungumzia usajili wa pikipiki ambao uliisha Desemba 31,
2015, Kidata alisema TRA imeongeza muda wa mwezi mmoja kutoa fursa kwa
ambao hawajakamilisha usajili huo wafanye hivyo. Alisema TRA imechukua
uamuzi huo kwa kuwa usajili huo ulikumbwa na changamoto kadhaa ambazo
zilisababisha usajili kutokamilika kwa asilimia 100.
Created by Gazeti la HabariLeo.
Wednesday, 6 January 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment