Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
SERIKALI imekataa viwango vya nauli mpya vilivyopendekezwa na Kampuni
ya Uda Rapid Transit (UDA-RT), itakayotoa huduma ya usafiri wa mabasi
yaendayo haraka Dar es Salaam. Pamoja na kukataa imeweka bayana kuwa
viwango hivyo viko juu ambavyo wananchi wengi watashindwa kuvimudu.
Kauli hiyo ya serikali imetolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
ambaye pia ameagiza wizara zote zinazohusika kukutana haraka
iwezekanavyo na kujadili viwango vipya vya nauli vinavyoendana na hali
halisi ya maisha ya wananchi. “… sasa nataka mamlaka zote zilizohusika
wakutane na kuja na viwango vipya vya nauli kama huyu mwekezaji
ameshindwa aseme, Serikali inaweza kuendesha mradi yenyewe,” alisisitiza
Majaliwa.
Wizara na taasisi zilizoagizwa kukutana ni Wizara ya Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa (Tamisemi); Wizara ya Ujenzi na ya Uchukuzi;
Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) pamoja
na kampuni ya UDA-RT.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam muda mfupi baada ya
kurejea akitokea Ruvuma, alikokamilisha ziara yake ya kikazi jana,
alisema viwango hivyo vilivyopendekezwa na vinavyotarajiwa kujadiliwa na
Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) havifai na
havikubaliki.
Alisema Novemba 25, mwaka jana alitembelea mradi huo wa DART na
kumuagiza Katibu Mkuu wa Tamisemi, Mtendaji Mkuu wa DART pamoja na
Wakala wa Barabara (Tanroads) kupitia mfumo mzima wa uendeshaji wa mradi
huo, lakini hadi leo hakuna mpango wowote wa biashara uliowasilishwa
serikalini na UDA-RT.
Alisema pamoja na hayo, pia kampuni hiyo imeshindwa kuweka bayana
gharama za uendeshaji wa mradi huo, uliotakiwa kuanza rasmi Januari 10,
mwaka huu. Majaliwa alisema wakati kampuni hiyo ikishindwa kuweka wazi
mpango wake wa kibiashara, alishangaa juzi kusikia imewasilisha vi wango
vya nauli vilivyopendekeza ambavyo vilikuwa vya gharama ya juu.
“Kwa kukosekana tu gharama halisi za uendeshaji mradi, ni dhahiri
kuwa nauli zilizopendekezwa hazina uhalisia,” alisema. Kampuni hiyo
ilipendekeza safari kwenye njia kuu kuwa Sh 1,200 na safari katika njia
kuu na pembeni kuwa Sh 1,400 na wanafunzi nusu ya nauli hizo. “Gharama
hizi ni kubwa mno.
Mradi huu unalenga kumlinda na kumsaidia mwananchi wa kawaida,
wakiwemo watumishi wa umma ambao wengi wao wamejenga pembezoni mwa mji
kuweza kusafiri kutoka maeneo ya pembeni hadi katikati ya jiji kwa
gharama nafuu na kwa urahisi na si kumkandamiza,” alisema Majaliwa.
Alisema kipato cha wananchi kwa ujumla wakiwemo watumishi wa umma,
bado si kikubwa. Alitoa mfano kwamba, mtumishi anayelipwa mshahara wa Sh
250,000 kwa mwezi, kwa nauli iliyopendekezwa pamoja na watoto wake,
fedha yote inaishia kwenye nauli.
Alisema kwa hali ilivyo, Serikali haiwezi kuridhia viwango hivyo
ambavyo ni wazi vitamkandamiza mwananchi badala ya kumsaidia. “Bado
tunayo nafasi ya kuendesha mradi huu, si lazima tuanze Januari 10 kama
ilivyopangwa, ni bora tuchelewe na kuanza tukiwa na viwango vya nauli
vinavyoridhisha badala ya kuanza na nauli hizi ambazo ni gharama kubwa
mno.”
Juzi Sumatra ilikutana na wadau kwa ajili ya kujadili mapendekezo
hayo ya nauli, ambayo hata hivyo yalipingwa na wadau wengi wa sekta ya
usafiri. Walishauri nauli iwe kati ya Sh 400 na Sh 500 kutimiza malengo
ya kusaidia wananchi wa kipato cha kawaida.
Pamoja na hayo wadau hao wakiwemo wananchi na Baraza la Walaji la
Sumatra (Sumatra CCC), walihoji sababu za mabasi hayo yanayobeba watu
wengi kwa safari moja na yanayotumia barabara zisizo na foleni, yatoze
nauli kubwa wakati dalad
Created by Gazeti La HabariLeo.
Wednesday, 6 January 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment