Madereva
wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es salaam wamesema watagoma
kuendesha magari hayo kufuatia uongozi wa mabasi hayo kuwapa mkataba wa
kazi usiokidhi mahitaji.
Baadhi ya mahitaji hayo ni mshahara mdogo wa shilingi laki 4 kwa mwezi tofauti na makubaliano ya awali ya shilingi laki 8.
Wakiongea
na Eatv leo, madereva hao wamesema pia wameshangazwa na kitendo cha
uongozi wa mabasi hayo kuwapa mkataba wa kazi bila ya kuwapatia nakala
yake jambo ambalo wamesema ni kinyume cha taratibu za ajira.
Madereva
hao ambao leo walikusanyika katika kituo kikuu cha mabasi yaendayo
haraka kilichopo eneo la Kamata wamesema tayari walishatangaziwa malipo
halisi kuwa ni shilingi laki 8 hivyo kitendo cha kusainishwa mkataba wa
malipo ya shilingi laki 4 hawakubaliani nacho.
Credit;Mpekuzi blog
0 comments:
Post a Comment