Baraza la uhusiano
mwema la kiislamu nchini Marekani limemtaka mgombea wa urais kwa tiketi
ya chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump, kuomba msamaha kwa
kuamrisha mwanamke wa dini ya kislamu kufurushwa kutoka kwa mkutano
wake wa kisiasa.
Rose Hamid alilalamikia wito wa bwana Trump wa kuweka marufuku ya muda kwa waislamu wanoingia nchini Marekani.Wafuasi wa Trump walipoketi, mwanamke huyo alisimama kwa ukimya, huku akivalia vazi lililokuwa na maandishi, salaam. Nimekuja kwa amani.
Umati uliyokuwemo ulifanya kelele za kejeli na maafisa wa usalama wakamwondoa.
Bi Hamid mwenye umri wa miaka 56 na ambaye anafanya kazi ya huduma katika kampuni ya moja ya ndege ,baadaye aliamrishwa na afisa mmoja wa usalama kuondoka.
Alizomwa wakati alipokuwa akifurushwa katika mkutano huo.
Chanzo BBC Swahili.
0 comments:
Post a Comment