Korea Kaskazini inasema kwa mara ya kwanza imefanikiwa kufanya majaribio ya bomu la nguvu ya maji{hydrogen}.
Tangazo
hili limetolewa na runinga ya taifa baada ya kusikika mitetemeko ya
kipimo cha tano nukta moja, karibu na eneo kuliko na kinu cha nyukilia.
Wataalamu wa Marekani wanafanya uchunguzi ikiwa yalikua majaribio ya
bomu hiyo au ilikua zana nyingine ya nyuklia isiyokuwa na nguvu.Mwandishi wa BBC anasema bomu la nguvu ya maji lina uwezo mkubwa wa mulipuko ikilinganishwa na mabomu mengine yenye madini ya Plutonia ambayo Korea kaskazini imefanya majaribio katika miaka ya awali.
Mamkala za Pyongyang zimefanyia majaribio mengine matatu ya kinyukilia katika eneo kulikofanywa majaribio ya sasa kwa kipindi cha miaka kumi.
Created by BBC Swahili.
0 comments:
Post a Comment