Na Maneno Selanyika, Dar es Salaam
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza
kushuka kwa bei ya mafuta ya Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa,
ikilinganishwa na bei ya mwaka jana.
Taarifa iliyotolewa na EWURA jana na kusainiwa na Mkurugenzi Mkuu
wake, Felix Ngamlagosi, ilieleza kuwa bei hiyo elekezi itaanza kutumika
kuanzia leo Januari 6.
Ngamlagosi alitaja sababu mojawapo ya kupungua kwa bei za mafuta ni
kushuka kwa bei za mafuta katika soko la dunia, pamoja na kushuka kwa
gharama za usafarishaji na uletaji wa bidhaa hizo.
“Bei za jumla na rejareja kwa mafuta ya aina hizo, zimeshuka
ikilinganishwa na toleo lililopita la Desemba 2 mwaka jana ambapo kwa
mwezi huu bei za rejareja kwa mafuta hayo zitapungua kama ifuatavyo
Petroli Lita 79 itapungua kwa asilimia 4.01, Dizeli lita 76 punguzo ni
asilimia 4.20 na Mafuta ya taa lita 66 itakuwa asilimia 3.73,” ilisema
taarifa hiyo.
Katika taarifa hiyo, mamlaka hiyo imewataka wananchi kuzingatia mambo
muhimu ambayo ni pamoja na kulinganisha bei hizo za mafuta na zile za
toleo la Desemba mwaka jana ambazo zilikuwa Petroli Sh 79.19 kwa lita
sawa na asilimia 4.23, Dizeli Sh 76.49 kwa lita sawa na asilimia 4.45 na
Mafuta ya Taa Sh 65.86 kwa lita sawa na asilimia 3.97, Alisema kwa
mujibu wa Sheria ya Mafuta ya Mwaka 2008, bei za bidhaa hizo zitaendelea
kupangwa na soko.
“EWURA itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei
kikomo za bidhaa za mafuta. Taarifa hizi zina lengo la kuwasaidia wadau
kufanya maamuzi stahiki kuhusu manunuzi ya bidhaa za mafuta.
Created by Gazeti la Mtanzania
Wednesday, 6 January 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment