Naib Waziri wa Aridhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Anjelina Mabula (kushoto) na viongozi wa
Serikali ya Wilaya ya Morogoro wakisoma mabango yaliyoshikiliwa na
wakazi wa mtaa wa Malamo, wilaya ya Mvomero.
WANANCHI wa Kitongoji cha Malamo, kilichopo katika Kijiji cha Wami
Sokoine, wilayani Mvomero, mkoa wa Morogoro waliobomolewa nyumba zao
baada ya kudaiwa kujenga ndani ya hifadhi ya msitu wa kuni uliopo
wilayani humo wamezua kizaazaa kwa kuzuia msafara wa Naibu Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Anjelina Mabula wakimtaka
awasikilize kero zao.
Baadhi ya wananchi hao waliamua kusimama bila woga katikati ya
barabara kuu ya Morogoro- Dodoma wakiwa na mabango yaliyokuwa na ujumbe
wa kumtaka Naibu Waziri huyo asimame juzi katika eneo la Mkundi na
awasikilize kero zao.
Mara baada ya Naibu Waziri huyo kusimama na kuelekea pembezoni mwa
barabara kuu hiyo ili kuwasikiliza kero zao wananchi hao walidai
wamebomolewa nyumba zao kwa njia isiyo halali na kwamba walikuwepo
katika kitongoji hicho kilichopo katika kijiji cha Wami Sokoine eneo la
wilaya ya Mvomero kwa muda mrefu kutokana na baraka ya serikali ya
kijiji hicho.
Walidai kuandika barua kwa serikali ya wilaya na mkoa wa Morogoro
mwaka 2013 na Desemba mwaka jana za kuomba serikali ibatilishe eneo hilo
linaloelezwa kuwa ni hifadhi ya msitu wa kuni liweze kuwa la makazi ili
kupunguza uhaba wa maeneo ya makazi kwa wananchi wa manispaa .
“Unakuomba Naibu Waziri utambue kuanzia sasa kuwa sisi zi wavamizi
bali tumeonewa,” alisema mkazi huyo kwa kwa niaba ya wenzake. Akijibu
hoja za wananchi hao, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, Anjelina Mabula alisema aliamua kusimama kuwasikiliza kwa kuwa
yeye ni kiongozi na ni wajibu wake kusikiliza kero zao na baada ya
kusikiliza kero zinazowakabili aliwataka wananchi hao wawe na subira kwa
vile suala la maombi yao yaliyowasilishwa kwa viongozi wa ngazi ya
wilaya na mkoa bado yanafanyiwa kazi.
Mabula aliwataka pia waende katika ofisi za halmashauri ya Manispaa
na wilaya kupata viwanja vilivyopimwa na vibali vya kujenga makazi yao
huku wakisubiri muafaka wa suala lao.
Chanzo Gazeti la HabariLeo.
Sunday, 10 January 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment