Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
JENGO la Polisi Makao Makuu, jijini Dar es Salaam limenusurika
kuteketea kwa moto baada ya kutokea hitilafu ya umeme katika jengo hilo.
Moto huo uliwashtua wafanyakazi wa polisi makao makuu ambao walikuwa wakikimbizana kutoka nje ili kunusuru maisha yao.
Akizungumzia tukio hilo, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Bulimba,
alisema moto huo ulianzia katika dari kwenye jengo la ghorofa ya nne
ambao baada ya kuanza kuungua moto na moshi kuenea katika baadhi ya
maeneo ya jengo hilo.
Alisema wafanyakazi walipoona cheche katika ghorofa hiyo ndipo
walipoanza kutoa taarifa kwa wafanyakazi wenzao na kutoka nje ili
kujiokoa.
“Moto ulianzia katika dari ambapo kulikua kunatoa cheche nyingi na
baadae tumetoa taarifa katika kikosi cha ulinzi na uokoaji zimamoto
wamekuja kuuzima,” alisema.
Alisema moto huo haujaleta madhara yoyote kwa wafanyakazi wala katika vitu vyovyote vya ofisi.
“ Tunashukuru kikosi cha zimamoto kufika mapema na kwa wakati hata
hivyo watu walikuwa wakisema tulikuwa katika mazoezi lakini si hivyo
bali ni moto tu na tayari umedhibitiwa,” alisema.
Chanzo Mtanzania.
Wednesday, 6 January 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment