Monday, 1 February 2016

Tagged Under:

Ted Cruz amshinda Trump mchujo wa Iowa

By: Unknown On: 21:17
  • Share The Gag
  • Trump alikuwa akiongoza kwenye kura za maoni
    Seneta wa Texas Ted Cruz ameshinda mchujo wa uchaguzi wa mgombea wa uchaguzi wa Republican katika jimbo la Iowa, Marekani.
    Huo ndio mchujo wa kwanza katika uchaguzi wa urais wa 2016 ambao utafanyika baadaye mwezi Novemba.
    Mfanyabiashara Donald Trump alikuwa akiongoza kwenye kura za maoni kabla ya kura kupigwa lakini sasa dalili zinaonyesha kwamba atakuwa wa pili.
    Seneta wa Florida Marco Rubio anaonekana kufanya vyema kuliko ilivyotarajiwa, na huenda akamaliza nambari tatu.
    Kura za mchujo wa chama cha Democratic bado zinahesabiwa.
    Asilimia 85 ya kura ambazo zimehesabiwa zinaonyesha pengo kati ya

    Hillary Clinton na mshoshialisti wa chama cha Democratic Bernie Sanders ni 1% pekee.
    Akizungumza baada ya matokeo kujulikana, Marco Rubio amempongeza Bw Cruz na kusema ndiye mgombea ambaye anaweza kuunganisha chama cha Republican ambacho kimegawanyika.
    Bw Trump amempongeza Bw Cruz Dakika chache baadaye, Bw Trump alipanda jukwaani katika ukumbi mwingine na kumpongeza seneta huyo wa Texas, na kusema anaridhika kumaliza katika nambari mbili.
    Wagombea wawili wamejiondoa kinyang’anyironi.
    Duru za karibu na mgombea wa Democratic Martin O'Malley, aliyekuwa gavana Maryland, zimeambia BBC kwamba atasitisha kampeni yake, na kufanya ushindani mkali sasa kuwa kati ya wagombea wawili.
    Upande wa Republican, gavana wa zamani wa Arkansas Mike Huckabee ameandika kwenye Twitter kwamba atasitisha kampeni yake.

    Chanzo BBC Swahili.

    0 comments:

    Post a Comment