Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Kintinku wilayani Manyoni Mkoa wa Singida,
Mahando Sabato amefikishwa Mahakama ya Wilaya ya Manyoni na Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kwa tuhuma ya kuomba na
kupokea rushwa ya Sh350,000.
Ilidaiwa kuwa mshtakiwa huyo, alifanya kitenda hicho ili amsaidie mlalamikaji kuifuta kesi iliyokuwa ikimkabili kijana wake.
Mkuu
wa Takukuru, Wilaya ya Manyoni, Michael Sanga alidai kuwa Desemba 30,
mwaka jana, ofisi yake ilipokea taarifa kutoka kwa mlalamikaji (jina
limehifadhiwa), kuwa hakimu Sabato alikuwa akimuomba rushwa hiyo ili
afute kesi ya wizi wa Sh400,000 iliyokuwa ikimkabili kijana wake.
Sanga
alidai kuwa katika kufanikisha azma yake ya kula rushwa, hakimu huyo
alifuta dhamana ya mtuhumiwa huyo na kuamuru apelekwe mahabusu ya Gereza
la Wilaya ya Manyoni, kwa siku 21 wakati akiendelea na mambo mengine.
“Baada
ya kubaini kwa hakimu Sabato amedhamiria kwa kiwango kikubwa kupokea
rushwa hiyo, tuliweka mtego katika eneo la kituo cha mabasi cha
Kintinku, ndipo tukamkamata akiwa na fedha za mtego huo wa hongo,”
alidai Sanga.
Mshtakiwa huyo yupo nje kwa dhamana hadi Februari 17, kesi yake itakafikishwa mahakamani kusomewa maelezo ya awali.
Wakati
huohuo, Takukuru imemfikisha kortini Ofisa Elimu Wilaya ya Kyela mkoani
Mbeya, Prochesius Mguli kujibu tuhuma ya kughushi nyaraka za malipo kwa
walimu 22 wa shule za sekondari wilayani humo.
Akisoma mashtaka
dhidi ya mshtakiwa huyo katika Mahakama ya Wilaya ya Kyela, Ofisa wa
Takukuru , Thomas Msuta alidai kuwa kati ya Agosti 18 na 30 mwaka 2012,
mshtakiwa alighushi majina ya walimu hao, alidai walihudhuria semina na
kuwalipa Sh3.3 milioni.
Msuta alidai mshtakiwa huyo katika ripoti yake alighushi saini za walimu hao wakati hawakushiriki kwenye semina.
Mshtakiwa yupo mahabusu baada ya kushindwa kukamilisha masharti ya dhamana.
Hakimu, Jacob Ndila aliahirisha kesi hiyo hadi Februari 17 itakapotajwa tena.
Credit;Mpekuzi blog
0 comments:
Post a Comment