07:44 Kuna ripoti kwamba baadhi ya watu wanaotumia simu kuingia mitandao ya kijamii ya Twitter na Facebook wanatatizika. Lakini WhatsApp inafanya kazi.
07:30 Upigaji kura ulifaa kuanza saa moja asubuhi lakini katika vituo vingi, licha ya wapiga kura kujitokeza, shughuli yenyewe haijaanza na wapiga kura wanalalamika. Katika kituo cha Kamwokya Central Market, vifaa vya kupigia kura vinaingizwa kituoni pole pole. Mwangalizi wa uchaguzi wa Jumuiya ya Madola Rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo amekuwa katika kituo hicho.
07:09 Tuangalie takwimu muhimu kuhusu uchaguzi wa Uganda unaofanyika leo.
Takwimu muhimu | |
---|---|
Wagombea urais | 8 |
Maeneo bunge | 290 |
Vituo vya kupigia kura | 28,010 |
Wapiga kura waliosajiliwa | 15,277,196 |
06:40 Wapiga kura wameanza kufika katika vituo vya kupigia kura. Hapa ni katika kituo cha Kalangala, katika kisiwa kilichoko katika Ziwa Victoria.
06:30 (Saa za Afrika Mashariki) Hujambo! Twatumai umeamka salama. Karibu kwa habari za moja kwa moja kuhusu uchaguzi mkuu wa Uganda.
Wapiga kura 15 milioni nchini Uganda leo wanafika vituoni kupigia kura viongozi wao, kinyang'anyiro cha urais kikivutia wagombea wanane.
Vituo vya kura vitafunguliwa saa moja asubuhi na kufungwa saa kumi alasiri.
Chanzo BBC Swahili.
0 comments:
Post a Comment