Wednesday, 17 February 2016

Tagged Under:

NEC wakanusha mchakato kura ya maoni

By: Unknown On: 22:18
  • Share The Gag

  • Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ramadhani Kailima

    TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imekanusha taarifa zilizoandikwa na baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuwa mchakato wa Kura ya Maoni ya Katiba Inayopendekezwa, uko mbioni kuanza.
    Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ramadhani Kailima imebainisha kuwa yapo mambo kadhaa yanayohitajika kukamilika kabla ya kuanza rasmi kwa mchakato huo wa Kura ya Maoni ya Katiba Inayopendekezwa.
    Kailima alisema kuwa Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar ambao uliahirishwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) ni moja ya mambo ambayo yanahitajika kukamilika ili kuiwezesha Zanzibar kushiriki katika mchakato huo.
    “Mambo mengine yanayohitajika kukamilika ili kuwezesha kuanza kwa mchakato huo wa Kura ya Maoni ya Katiba Inayopendekezwa ni pamoja na kukamilika kwa uchaguzi wa ubunge katika Jimbo la Kijitoupele huko Zanzibar ili kukamilisha idadi ya wabunge 50 wa Jamhuri ya Muungano kutoka Zanzibar,” alieleza Kailima.
    Aidha, taarifa hiyo pia imebainisha kuwa suala lingine ambalo halijakamilika ni kupatikana kwa wabunge watatu wa Viti Maalumu ambao kupatikana kwao ni lazima Jimbo la Kijitoupele Zanzibar likamilishe uchaguzi wake na kumpata mbunge.

    Chanzo HabariLeo.

    0 comments:

    Post a Comment