WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa jana jioni (Ijumaa, Februari 19, 2016) alikagua
bandari ya Tanga na kumtaka Mkuu wa Bandari ya Tanga (Port Master), Bw.
Henry Arika amletee maelezo juu ya ukiukwaji wa manunuzi ya tishari
ifikapo leo (Jumamosi) saa 6 mchana.
Waziri
Mkuu ambaye aliwasili Tanga jana mchana ili kushiriki mazishi ya baba
mzazi wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Bi. Ummy Mwalimu yaliyofanyika kwenye makaburi ya Mchukuuni, Tanga,
aliamua kuzuru bandari hiyo kabla ya kuelekea uwanja wa ndege akiwa njia
njiani kurejea Dar es Salaam.
Katika
ziara hiyo fupi, Waziri Mkuu alikataa kuingia ofisini (bandarini) na
akataka apelekwe mahali tishari tatu za bandari hiyo zilipo.
Katika
maswali aliyoulizwa na Waziri Mkuu, Bw. Arika alikiri kuwa matishari
hayo hayafanyi kazi kama inavyotakiwa kwa sababu yanasubiri kusukumwa na
tugboat (meli ndogo).
"Nataka
kesho saa 6 mchana uniletee barua yenye maelezo ni kwa nini mlinunua
tishari tatu ndogo badala ya mbiili kubwa wakati mnajua Serikali
ilitenga Dola za Marekani milioni 10.113 kwa ajili ya kununua tishari
mbili zenye uwezo wa kujiendesha zenyewe (self propelled) "
“Nataka
maelezo ni kwa nini mlizinunua tangu mwaka 2011 lakini zimekaa bila
kufanya kazi hadi Novemba mwaka jana? Na kwa nini mnaendelea kutumia
hela ya Serikali kwa kukodisha tishari kutoka Mombasa badala ya
kutengeneza za kwenu au kufundisha vijana wa Kitanzania? Kwani tunao
wahitimu wangapi wa fani hii?" alihoji Waziri Mkuu.
"Taarifa
nilizonazo ni kwamba moja ya tishari lilidondoka baharini mkaenda
kutafuta huko na kulivuta hadi hapa ndiyo maana yameshindwa kufanya kazi
inavyotakiwa," aliongeza.
Katika majibu yake, Bw. Arika alisema wao waliagiza tishari hizo kupitia ofisi ya Bandari makao makuu ambayo iko Dar es Salaam.
"Pia wakati zinaagizwa sikuwepo hapa Tanga. Nimekuja mwishoni mwa mwaka jana," alisema Mkuu huyo wa Bandari ambaye inaelezwa alitokea Mamlaka ya Bandari Dar es Salaam.
Katika
hatua nyingine, Waziri Mkuu alimtaka Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Bibi
Mwantumu Mahiza awaite watu wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Mamlaka ya
Bandari na Jeshi la Polisi wakae na kutafuta mbinu za kudhibiti njia za
panya zinazotumika kupitisha sukari ya magendo.
"Mkuu
wa Mkoa simamia hawa watu, msaidiane kudhibiti uingizaji wa sukari kwa
njia za panya. Kuna majahazi yanaleta sukari kutoka Brazil. Mheshimiwa
Rais amepiga marufuku uingizaji wa sukari kutoka nje ili viwanda vyetu
vya ndani viweze kuongeza uzalishaji. Dhibitini bandari zote ndogondogo
hadi Pangani," alisema Waziri Mkuu.
Alisema
changamoto inayoikabili Serikali ni kwamba hata Shirika la Viwango
Tanzania (TBS) au Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) hawawezi kuzikagua
sukari hizo na hazijulikani ubora wake licha ya kuwa zinafika kwa
walaji.
Waziri
Mkuu, Kssim Majaliwa akiongozwa na Mkuu wa Bandari ya Tanga , Henry
Arika (kulia kwake) kukagua bandari hiyo Februari 19, 2016.
Matishari
matatu ambayo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametaka apewe maelezo kwa
maandishi kuwa ni nani aliyeidhinisha mchakato wa manunuzi yake bila
kuzingatia viwango na ubora uliokusudiwa na serikali. mheshimiwa
Majaliwa alifanya ziara katika bandari ya Tanga Februari 19, 2016.
(Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
Credit;Mpekuzi blog
0 comments:
Post a Comment