Mgombea kiti wa
chama cha Republican katika uchaguzi ujao wa urais nchini Marekani
Donald Trump ameshinda kura ya mashinani katika jimbo la Carolina
Kusini.
Bwana Trump ambaye awali mwezi huu, alishinda katika jimbo
la New Hampshire, amepata kura nyingi huko Carolina Kusini huku
wapinzani wake Ted Cruz na Marco Rubio wakimfuatia kwa karibu.Kutokana na matokeo mabaya ya gavana wa zamani wa Florida, Jeb Bush, kakake aliyekuwa Rais wa Marekani George W. Bush, amejiondoa katika kinyanganyiro hicho.
Awali mgombea kiti hicho kwa chama cha Democrats Bi Hillary Clinton ameibuka mshindi katika kura ya mashinani eneo la Nevada, na kubwaga mpinzani wake Bernie Sanders.
Chanzo BBC Swahili.
0 comments:
Post a Comment