Waziri wa kilimo, uvuvi na mifugo MWigilu Nchemba (kushoto) mkuu wa wilaya wa Mvomero, Suleiman Sadick Murad na wanakijiji wa Kambara wilayani
humo wakiangalia mbuzi, kondoo na ndama zaidi ya 80 wa mfugaji wa jamii
ya kimasai (kulia), Ketepoi Nuru waliouawa kwa kuchinjwa na walinzi wa kijadi wa mwano baada ya kudaiwa kula mazao ya mmoja wa wakulima wa eneo hilo.
WAZIRI wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba ameiagiza Polisi
wilayani Mvomero na Mkoa wa Morogoro kuwasaka na kukitia mbaroni kikundi
cha ulinzi wa jadi kiitwacho Mwano kwa tuhuma za kuua mbuzi na kondoo
wapatao 80.
Mifugo hao ni kati ya 200 waliokuwa wakimilikiwa na mwanamke mjane wa
jamii ya wafugaji wa Kimasai, Ketepoi Nuru ama Christina Nuru, mkazi wa
Kijiji cha Kambara wilayani Mvomero, Morogoro.
Waziri alitoa agizo hilo katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha
Dihombo, Kata ya Hembeti baada ya kujionea baadhi ya mifugo iliyokuwa
imekatwa kwa mapanga, baadhi ikiwa imekufa na mingine ikiwa na majeraha.
Tukio hilo lilijiri Februari 8, mwaka huu baada ya kikundi cha Mwano
chenye watu takribani 50 kuvamia nyumbani kwa mwanamke huyo na
kuishambulia mifugo hiyo zizini kwa kuikata mapanga.
Mwigulu alisema kitendo kilichofanyika ni cha kinyama na hakifai
kabisa kuvumiliwa. Kikundi hicho baada ya kuvamia nyumbani kwa mwanamke
huyo na kuua na kujeruhi mifugo 80, inaelezwa kwamba walichukua wengine
zaidi ya 50 kwa bajaji na pikipiki na kutoweka nao.
Chanzo Habari Leo.
Tuesday, 9 February 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment