WATU
wawili akiwemo Meneja Vipindi wa kituo cha televisheni cha East Africa
(EATV), Lidya Igarabuza (37) wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka mawili likiwemo la kuishi
nchini bila kibali.
Igarabuza
ambaye ni mtanzania na raia wa Kenya, David Wachila (36), ambaye
anadaiwa kuwa ni DJ wa muziki katika kituo hicho cha televisheni,
walifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashitaka mbele ya Hakimu
Mkazi Mkazi, Kwey Rusema.
Wakili
wa Serikali kutoka Idara ya Uhamiaji, Khadija Masoud alidai kuwa
Februari 25, mwaka huu katika maeneo ya Mikocheni A, Wachila akiwa raia
wa Kenya, alikutwa akiishi nchini bila kibali jambo ambalo ni kinyume
cha Sheria za Uhamiaji. Katika mashitaka yanayomkabili, Igarabuza
anadaiwa kumhifadhi Wachila jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
Inadaiwa
Februari 25, mwaka huu huko maeneo ya Mikocheni, Igarabuza alikutwa
amemhifadhi Wachila huku akijua jambo hilo ni kinyume cha sheria.
Washitakiwa walikiri kutenda makosa hayo.
Wakili
Masoud aliiomba mahakama ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kuwasomea
maelezo ya awali. Hakimu Rusema aliahirisha kesi hiyo hadi Machi Mosi,
mwaka huu. Igarabuza aliachiwa kwa dhamana wakati mshitakiwa Wachila
akirudishwa rumande kwa kukosa wadhamini.
Credit; Mpekuzi blog
0 comments:
Post a Comment